HabariNews

Ongezeko la Dhuluma ya Watoto lashuhudiwa kaunti ya Kwale, Wazazi Wakilaumiwa kwa Utepetevu 

Idara ya watoto eneo la Lungalunga kaunti ya Kwale imetaja kukithiri kwa Visa vya dhulma ya watoto katika eneo hilo.Hii ni baada ya Visa 40 vya wazazi kutelekeza majukumu ya watoto wao kuripotiwa kwa muda wa miezi 3 huku.

Inaarifiwa kuwa Visa 14 vya watoto wenye umri wa chini ya Miaka 18 kuozwa mapema vimeripotiwa huku Visa 358 vikirekodiwa vya dhuluma za kunajisiwa  kwa muda wa miaka 3 sasa.

Akizungumza wakati wa kuadhimisha siku ya kulinda haki za watoto katika eneo la Mshiu, Afisa wa watoto eneo la Lungalunga Elizabeth Kariuki aliitaka jamii kukomesha dhulma dhidi ya watoto hao na badala yake kulinda haki zao kwa mjibu wa katiba.

Tumeona hii dhuluma zimekuwa juu sana, kwahio tumeenda tukiwa tunatafuta data yetu tukapata takribana ya miaka mitatu visa ambavyo vimekuwa Lungalunga ni 358, hawa ni watoto amabo wamedhulumiwa kingono. Hapo tuko na kazi ya kufanya, na hii kazi itakuwa rahisi kama tukishirikiana, itakuwa rahisi kama hivi visa vitaripotiwa kwa wakati.” Alisema.

Mkurugenzi wa shirika la Kids care Kenya George Baya ameitaka serikali ya kitaifa ile ya kaunti pamoja na mashirika mbalimbali kuungana na kutafuta mwafaka wa kukomesha dhulma kwa watoto.

Sababu ambazo ziko ni ukosefu wa kujua haki za watoto ambazo zinatakikana zitimizwe katika jamii, kulingana na kwamba watu hawana habari hizo unakuta jambo linatendeka na wanaona kwamba wasuluhshe pale mitaani na linaleta sasa kwamba mtoto anadhulumuka na ndio maana tunaleta hamasisho ili waweze kujua wao pia nao jukumu lao ni lipi katika kulinda haki za mtoto,” alisema Baya

Kwa upande wake gavana wa Kwale Fatuma Achani ameitaka idara ya mahakama kuwachukulia hatua kali za kisheria wazazi wanaoshirikiana na washukiwa wa dhulma za watoto ili kuhakikisha watoto wanapata haki.

Tutaendelea kuzungumza na mahakama ili wapeane mfano kwa wale ambao wanakiuka sheria. Mahaka ikitilia mkazo haya maneno, wakipeana hukumu kwa muda mfupi mimi ninaimani kuwa kila mtu atafunga mlango wake pale nyumbani. Chiefs, Assistant chiefs yale mambo ya kuwa kesi zafichwa pale chini, zasuluhishwa pale chini pia nayafe, kwahivyo pia twawaomba mutusaidie pia pale hini zile kesi ziweze kutoka pale chini zifike pale juu ili mtoto awezekupata haki yake.” Alisisitiza Achani.

BY BINTIKHAMIS MOHAMMED