HabariNews

HATARI! Wakazi Lamu Wahangaishwa na Mafuriko kutokana na Mvua Kubwa Inayoendeea Kunya Pwani

Maeneo ya Lumshi, Jipendeni,  Amkeni miongoni mwa maeneo mengine yamesombwa na mafuriko katika Kaunti ya Lamu yaliosababishwa na mvua kubwa inayoshuhudiwa Maeneo mbali mbali Pwani na kote nchini.

Naibu wa Gavana wa Kaunti ya Lamu Raphael Munywa aliyathibitisha haya akisema kuwa maeneo mengi yamo hatarini kusombwa na mafuriko na  kushinikiza wakaazi kuhamia maeneo ya juu ili kuepuka kusombwa na mafuriko hayo.

Munywa alitahadharisha wakaazi hao ambao  mara kwa mara wamekuwa wakiomba msaada kila wanapopatikana na majanga hasa mafuriko akisema kwamba ni bora zaidi kuhamia sehemu ya juu kabla ya majanga hayo kuwaathiri zaidi.

Mvua imekua nyingi maji tunapata kilio, maeneo ya lumes, maeneo ya amkeni, maeneo ya jipendeni tayari wananchi wameathirika ni vizuri pia musonge kidogo kwa maeneo ambayo yako juu musije mkasombwa na maji. Nakuna sehemu zingine pia sijataja kwahivyo tujaribu kusonga pahali pajuu tusiseme serikali ikowapi wanisaidie, lakini nimekuambia saii musonge” Alisema

 Kwa upande wake Kamishna wa Kaunti ya Lamu Lius Rono aidha aliwataka wakaazi wanaoishi maeneo ya chini kuamia maeneo salama haraka iwezekanavyo ili kuepuka mafuriko ya mvua kufuatia mto Tana kuvunja kingo zake.

Kamishna huyo alieleza hofu yake kutokana na mto huo akisema kwamba maji yake hayaingii baharini hivyo basi vijiji kama Lumshi, Moha, Chalaluma, Didewaribe huenda vikasombwa na mafuriko hayo.

Niwaambie wale watu wanaoishiu katika maeneo ya mafuriko mujaribu kutoka hapo kwa ajili ya vile mto Tana umeanza kuvunja kingo zake, hio maji yam mto Tana haiingii baharini inazuiliwa. Sehemu kama Lumshi, Moha, Chalaluma, Didewaribe, Bangani wasonge upande wa juu” Alisisitiza Kamishna

BY NEWS DESK