HabariNews

IMF Yatoa Shilingi bilioni 142.8 kwa Taifa la Kenya

Shirika la Kimataifa la Fedha, IMF limetoa fedha takriban shilingi bilioni 142.8. Shirika hilo limefikia makubaliano ya kuwezesha upatikanaji wa haraka wa awamu, kiasi cha dola milioni 682.3  na kuboresha mpango wa sasa wa ukopeshaji kwa dolla milioni 938,  shirika hilo limesema.

IMF ilishikilia kwamba kutolewa kwa mgao huo wa fedha unatokana na uhusiano mwema kati ya taifa la Kenya na shirika hilo huku kenya ikionyesha nia ya kulipa mkopo wake kwa wakati.

Mkopo huo unajiri katika kipindi taifa linakabiliana na changamoto kubwa ya uhaba wa fedha za kufadhilia miradi yake kwa kukosa uhakika wa kupata ufadhili wa fedha kabla ya muda wa kulipa deni la dola bilioni 2 za Eurobond kukamilika kufikia Juni 2024.

Fedha hizo huenda zikaleta afueni kwa taifa hili ambapo tayari linakumbwa na malimbikizi ya madeni yaliyoathiriwa na janga la covid-19  na ukame wa mara mara kutokana na mabaliko ya tabianchi.

Kuimarika kwa hali ya ufadhili wa kimataifa kwa uchumi wa mipakani na mivutano ya kijiografia ya kimataifa inazidisha changamoto,” alisema Mkuu wa misheni, Haimanot Teferra.

Kulingana na mshiriki wa soko hilo, Ufadhili mpya wa IMF pamoja na fedha zinazotarajiwa kutoka kwa Benki ya Dunia na benki za kikanda kama Afrexim, utaruhusu Kenya kulipa deni lake bila kumaliza akiba yake ya fedha.

Mpango MPYA wa fedha wa IMF pamoja na msaada kutoka kwa banki kuu ya dunia na itawawezesha Kenya kulipa madeni yake.

Kenya itakua na sifa ya kukopeshwa zaidi,” alisema mdau huyo wa soko.

BY REUTERS