HabariNews

Maelfu ya Vyeti vya Kuzaliwa vyasalia Ofisini Kilifi

Maelfu ya vyeti vya kuzaliwa vinasalia katika ofisi ya usaliji wa vyeti hivyo mjini Kilifi bila kuchukuliwa na wenyewe licha ya wakazi kutuma maombi ya kutaka vyeti hivyo.

Tangu mwezi wa tatu mwaka huu kama ofisi tumetoa vyeti elfu 600 na vyeti vingi vipo ofisi ya huduma centre na tunaendelea kutuma jumbe fupi kwa wote waliotafuta vyeti hivyo ili kuwapunguzia mzigo wa kutembelea ofisi zetu mara kwa mara japo kuna wakaazi wachache wamejitokeza kuchukua vyeti vyao”.Alisema Mbui.

Vyeti hivyo vya kuzaliwa vinavyohitajika wakati wa kutafuta huduma mbali mbali za serikali, viliripotiwa kutochukuliwa kwake kwa kulemaza shughuli ya uchapishaji wa vyeti zaidi katika ofisi hizo.

Kulingana na mkurugenzi wa usajili wa watu Kaunti ya Kilifi Robert Mbui  ofisi hiyo imechapisha vyeti zaidi ya 6,000 tangu mwezi Machi mwaka huu 2023 alieleza kuwa vyeti vilivyosalia katika ofisi hiyo ni takriban 4,000.

Mbui alitoa wito kwa wakazi wa kaunti ya Kilifi kufanya hima ili kuchukua vyeti hivyo pindi wanapopokea jumbe fupi kuwataarifu kutayarika kwa vyeti hivyo.

Nawaomba wakaazi wawewaangalifu na madalali wanaojifanya wahudumu katika ofisi zetu.Aidha kila mtu aliyetuma maombi kutafuta cheti cha kuzaliwa atapata ujumbe mfupi kumtaarifu kwamba cheti chako kiko tayati”.Aliongeza Mbui

Mbui vile vile alielezea  mbinu ya kuwataarifu wote waliotuma maombi ya kutaka vyeti vya kuzaliwa kupitia ujumbe mfupi, ili kuepusha wakazi kupoteza muda kutembelea ofisi hizo bila mafanikio ya kupata vyeti hivyo.

Tahadhari hata hivyo ilitolewa kwa wote wanaotuma maombi kuwa waangalifu wasije wakahadaiwa na madalali wanaojifanya kuwa wafanyakazi katika ofisi hizo wasije wakajikuta pabaya.

BY ERICKSON KADZEHA