HabariNews

Watoto Mombasa waandamwa na ukatili wa Kijinsia na Gonjwa la Afya ya Kiakili

Ugonjwa wa Afya ya akili pamoja na ukatili wa kijinsia ulitajwa kuwa donda sugu miongoni mwa magonjwa mengine hususan kwa watoto katika Kaunti ya Mombasa.

Kulingana na mshauri wa maswala ya afya ya akili katika shirika la Collaborative Centre mjini Mombasa Hilda Akoth,  takwimu za hivi Karibuni kutoka wizara ya afya ya dunia(WHO) ilionyesha asilimia kubwa ya vijana wameathirika na afya ya akili kuliko wazee.

Akoth aliongezea kuwa kunahaja ya mashirika mbalimbali ya kijamii, serikali za kaunti na zile serikali kuu pamoja na makanisa kuungana ili kupigana na hali hiyo inayozidi kuwa kikwazo kwa watoto humu nchi.

Kwa sasa visa vya afya ya akili viko juu sana kwa watoto wadogo,Kulingana na takwimu za wizara ya afya ya kidunia WHO inaonyesha asilimia 46 wameathirika zaidi kuliko watu wakubwa,hii inaonyesha watoto wengi hupata ugumu wa kujieleza hivyo tukiwaleta pamoja na kuwaelimisha watajieleza na kuepukana na mitego hii”.Alisema Doroth.

Mkurugenzi mtendaji katika shirika la Together 4 Society Edwin Shamir aliitaka serikali kubuni mbinu mwafaka ili kuidhinisha somo la afya ya akili mashuleni kwa kuwaelimishaili wanafunzi hasa wenye umri mdogo kwani wako katika hatari kubwa zaidi.

Vilevile aliwaonya wazazi wanaowalazimisha watoto wao kuchagua masomo kinyume na yale mtoto mwenyewe anapenda kuwa ni kumnyima haki mtoto huyo pasi na kumshurutisha.

 

Vijana na watoto wameathirika zaidi na wako katika hali mbaya zaidi,ningependa kutoa ushauri na pendekezo kwa serikali kujumuisha elimu ya maswala ya akili ili kusaidia vizazi vyetu siku za usoni”.Alieleza Shamir.

Mchungaji wa kanisa la ACK St Emmanuel, Julius Ngala alitoa wito kwa serikali na mashirika mbalimbali kuungana ili kuokoa watoto hasa msimu huu wa likizo kwani watoto wengi hupitia mambo magumu pasi na kuhusisha wazazi wao, hali aliyoitaja kuongeza visa vya kujiua miongoni mwa visa vyengine.

Kama kanisa tumehusisha serikali,makundi ya kijamii na washikadau mbalimbali ili tuje pamoja na kutoa ushauri kwa watoto wetu hususan wanarika,na elimu hii iwe ya kiroho na hata mambo kama haya ya afya ya akili inayozidi kuwa kizungumkuti kwa watotot wetu”.Alisema Bishop Ngala.

By Simon Cephas.