HabariLifestyle

Uongozi wa Katoliki Kenya waainisha hatua ya Papa Francis kuhusu wapenzi wa Jinsia moja

Baraza la Maaskofu Kanisa Katoliki nchini KCCB limejitokeza kufafanua uamuzi wa kiongozi wa kanisa la katoliki humu nchini Papa Francis kuhusu mahusiano ya watu wa jinsia moja.

Mwenyekiti wa baraza hilo Martin Kivuva amesema hatua hiyo imezua mjadala mkali sio tu hapa nchini bali dunaini kote, na uamuzi huo haumanishi kwamba kanisa katoliki linaidhinisha ndoa za jinsia moja.

Kulingana naye msimamo wa kanisa katoliki haujabadilika japo amesema iwapo watu watahitaji kuombewa na kanisa basi hawana budi kufanya hivyo.

Amesema kuwa msimamo na ufahamu wa Kanisa Katoliki kuhusu ndoa kama muunganiko na sakramenti kati ya mume na mke bado haujabadilika licha ya tangazo hilo la Papa Francis.

Aidha Kivuva amesema kanisa katoliki li wazi na bila kusimamia misimamo yake na viongozi wake hawana haki kumhukumu binadamu yoyote.

Ikumbukwe kuwa Msimamo wa kiongozi wa kanisa la katoliki Papa Francis kuruhusu kuwabariki wapenzi wa jinsia moja umeendelea kuzua hisia miongoni mwa viongozi mbali mbali.

Aliyekuwa mwakilishi wa wadi ya Ganda kaunti ya Kilifi Abdulrahman Omar alikemea vikali hatua hiyo akisema huenda Kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki akakosa kuungwa mkono na waumini wake kutokana na maamuzi hayo kuwa kinyume na vitabu vitakatifu.

“Ndugu zetu wa Katoliki kuhusu kiongozi wao wanaomwamini kuwa yeye ameridhika kubariki wapenzi wa jinsia moja, mimi sidhani waumini wanapaswa kumuunga mkono. Hata wakiunga mkono, Mwenyezi Mungu amelilaani, vitabu takatifu haviungi mkono hilo ni laana,” alisema.

Kauli yao imejiri siku chache baada ya Papa Francis kuwaruhusu mapadri kuwapa baraka isiyo rasmi wanandoa wa jinsia moja.