HabariLifestyle

IG Koome aagiza Maafisa wa Polisi walio Likizoni kurejea kazini mara moja

Idara ya polisi haina nafasi kwa maafisa fisadi, ndiyo kauli yake Inspekta Jenerali wa polisi nchini Japhet Koome.

Akihutubia wanahabari nje ya makao makuu ya idara hiyo jijini Nairobi, Inspekta Mkuu huyo wa Polisi alibaini afisi yake I wazi na itashirikiana na Tume ya maadili na kupambana na ufisadi kukabiliana na ufisadi.

Koome amebainisha kuwa majukumu yote ya idara ya trafiki yatakuwa chini ya Naibu Inspkekta mkuu Mary Omare.

“idara ya polisi haina nafasi ya maafisa fisadi ,ofisi yangu ikowazi na itashirikiana na EACC, tumepanga maafisa wa polisi sio kama awali na sasa majukumu yaote yatakuwa chini ya Naibu mkuu Maryn Omare.” Alisema Koome

Kulingana na Koome Idara ya Polisi inashirikiana kikamilifu na Tume ya maadili na kupambana na Ufisadi EACC kuwafuatilia na kuwanasa maafisa fisadi walaji rushwa.

“Hiyo upuzi ingine haitakupleka popote ni shida tu utafungwa wakati EACC inakushika waweka kamera sasa utajifunika kwa maana umefanya makos ana familia yako inakuona na ni aibu” Aliongeza Bw. Koome

Wakati uo huo Idara hiyo ya Polisi iliagiza maafisa wote wa usalama walio katika likizo kurejea kazini mara moja ili kuzidisha doria msimu huu wa Krisimasi na Mwaka Mpya.

Koome vile vile amewaonya maafisa wa trafiki ambao watatumia vizuizi vya barabarani kuchukua hongo kwa njia yoyote kuwa watakabiliwa vikali na mkono wa sheria, huku akiwashauri madereva kuwa waangalifu barabarani.

“Tuhudumie wananachi iyo upuzi ya kurokota hasmini mia moja elfu moja haitakupeleka mahali,kizazi kijacho hakitanikumbuka na gari nililopeleka ama kiasi cha fedha nilichokuwa nacho badala yake kazi nzuri niliyofanya kwenye taifa hili,tuhakikishe kuwa nchi yetu iko imara.” Alisistiza Koome.

 

BY NEWSDESK