Uncategorized

Mackenzie Hachomoki! Ofisi ya DPP Yapata Stakabadhi Muhimu kuhusu Mauaji ya Shakahola

Afisi ya Kiongozi wa Mashtaka ya Umma nchini, ODPP imethibitisha kupokea stakabadhi rasmi kutoka Kwa idara ya upelelezi nchini DCI kuhusu mauaji ya Shakahola.

Katika taarifa Kwa vyombo vya habari Idara hiyo imebaini kuridhishwa na upelelezi huo unaolenga kushtaki washukiwa 95 kwa masktaka mbali mbali.

Kulingana na Idara hiyo upelelezi huo uligawanywa katika vitengo vitatu ikiwemo, upelelezi wa jinai, upelelezi wa ugaidi na upelelezi wa haki za watoto.

Kwenye upelelezi wa jinai mshukiwa mkuu Paul Mackenzie na wenzake wamepangiwa kushtakiwa na mauaji, mauwaji bila kukusudia pamoja na kusababisha maumivu Kwa miili kinyume na katiba.

Hata hivyo duru za habari zimefichua kuwa Mackenzie na wenzake watafikishwa katika mahakama kuu ya Malindi siku ya Jumatano Januari 17, kujibu mashtaka ya mauaji kabla ya kufikishwa Mahakama za Shanzu, Kilifi na Tononoka kujibu mashtaka yanayofungamana na masuala ya watoto.

BY JOSEPH YERI