HabariNews

Azimio ingali Imara licha ya semi tofauti za baadhi ya Viongozi, Asema Kalonzo

Kiongozi wa Chama cha WIPER, Kalonzo Musyoka amekanusha madai kuwa muungano wa Azimio unasambaratika.

Akihutubia wanahabari jijini Nairobi mnamo Jumanne, Kalonzo alisema tofauti za maoni katika upinzani haziwezi kuchukuliwa kama matatizo ndani ya muungano huo.

Hakuna kitu kama hicho kwamba eti Muungano wa Azimio la Umoja unasambaratika, ni hisia tu za watu na maoni yao wakidhania hivyo, lakini AZIMIO ipo imara kabisa na tumejitolea sana, japo tofauti za kimaoni na mtazamo zipo ila haimaanishi tumegawanyika. Azimio tuko imara na tunazidi kuunda upinzani imara ulio pamoja.” Alisema.

Kalonzo amepuuzilia mbali mgawanyiko katika mrengo huo akisisitiza kwamba vinara wenza katika muungano huo wangali imara na kwamba wamekuwa wakishirikiana katika harakati zao zote za upinzani.

Wakati huo huo Kalonzo alihimiza viongozi wa mrengo kutotekwa hisia na kuunga mkono kauli za kuishambulia zinazotolewa na viongozi wakuu serikalini.

Wakenya wameshawahi kuandamana kwa suala la gharama ya juu ya maisha na ukiongezea na suala hili la ukiukaji wa maagizo ya mahakama na kuhujumu muundo wa katiba basi unataka kujiingiza katika janga kubwa. Tunawahimiza wanachama wetu wa Azimio kutoruhusu kubebwa na wimbi hili la kuhujumu haki ya katiba na mahakama na wasiwe sehemu ya kuunga mkono uonhozi unaohujumu katiba.

Wengine wanahisi wanadhani wanapaswa kumfurahisha William Ruto hivyo wanatakuwa William Ruto zaidi ya Ruto mwenyewe, tafadhali muongozwe na sheria,” alisema.

BY MEDZA MDOE