Kenya siku ya Ijumaa Januari 26, ilijiunga na mataifa mengine ulimwenguni kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Nishati Safi.
Siku hiyo huadhimishwa kila tarehe 26 Januari kila mwaka kauli mbiu ya mwaka huu ikiwa ni mfumo endelevu wa nishati safi katika siku za usoni yaani (“Clean Energy: The transition to a sustainable future”.)
Hapa kaunti ya Mombasa maadhimisho hayo yalianza kwa matembezi ya amani kutoka Bustani ya Uhuru, eneo la Mapembeni hadi eneo la Treasury Square ambako kilele cha maadhmisho hayo yalifanyika kwa maonyesho mbalimbali na hotuba za viongozi.
Akiwahutubia wanahabari kabla kuanza kwa matembezi ya amani kuashiria mwanzo wa maadhimisho, Waziri wa uchukuzi kaunti ya Mombasa Daniel Manyara alisema wizara yake inafanya mazungumzo kuhakikisha utumizi wa nishati safi kwenye sekta ya usafiri.
“Tunahimiza wananchi kuzingatia kawi safi, kwa mikakati mbalimbali kama kutembea zaidi na kuepuka utumizi wa vyombo vya uchukuzi barabarani hasa magari ambayo yanachafua hewa. Pia tunahimiza kaunti ziweke mikakati ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi katika juhudi za kuweka mazingira bora kwa binadamu na wanyama kuishi.” Alisema.
Kwa upande wake Afisa mkuu wa idara ya maji, mali, asili na mabadiliko ya tabaia nchi kaunti hiyo Marian Mapenzi alisema kaam kaunti wampiga hatua kwa utumizi wa nishati safi ikiwemo kuingia kwenye makubaliano na kampuni ya Auto track na kutafuta mfumo endelevu wa kutumia pikipiki zinazotumia umeme kwa kuchaji batari za pikipiki hizo.
“Hatua tulizopiga kuhusu kawi safi ya Kijani tumeingia mkataba na washikadau na kuona vile jinsi tutatumia tuktuk kuwa na kawi ya kisasa na kubadili betri kuwa za kuchaji kwa umeme na pia vile pikipiki.” Alisema
Siku hii inaadhimishwa ili kujenga uhamasishaji na kubuni mpango madhubuti wa utekelezaji wa kupitisha nishati safi ambayo inanufaisha sayari hii na wanaoishi humu.
Kawi au nishati safi ni hatua mwafaka ya kupambana na mabadiliko ya hali ya hewa ambayo yamesababisha madhara makubwa katika bara la Afrika kwa miaka kumi na kusababisha njaa na hata vifo vya mifugo.
BY NEWS DESK