HabariNews

Idara ya afya Mombasa yaonya wanaokiuka matumizi ya vyandarua

Idara ya afya kaunti ya Mombasa imeagiza jamii  zinazoishi eneo hilo kujitokeza na kujisajili kwenye zoezi la ugavi wa vyandarua vilivyo na dawa  ili kujikinga dhidi ya maradhi ya malaria.

Wakizungumza wakati kongamano la kutoa hamasa kwa wadau mbali mbal katika sekta ya afya jijini Mombasa jumatatu tarehe 29 Januari, idara hiyo imetaka wakazi kujitokeza katika zoezi hilo ili kuhakikisha familia zinalindwa kutokana na maradhi hayo hatari.

Hata hivyo idara hiyo ilidokeza kuwa viwango vya maradhi ya malari vimepungua kwa asilimia kubwa hasa katika kaunti ya Mombasa.

Caroline Aguto afisa mkuu wa afya katika kitengo cha uhamasishaji kaunti ya Mombasa, alishauri raia kutotumia vyandarua hivyo kwa njia hisiyofaa kama kufuga kuku miongoni mwa matumizi mengine.

Aguto alisema maafisa wa afya watatumwa nyanjani na watakaopatikana wakikiuka matumizi ya vyandarua hivyo watachukuliwa hatua kali za kisheria.

By David Otieno