HabariNews

Watu 11 wamefariki na wengine zaidi ya 30 kujeruhiwa kufuatia ajali ya barabarani Kisumu

Watu 11 wamefariki na wengine zaidi ya 30 kujeruhiwa kufuatia ajali ya barabarani iliyotokea katika eneo la Othoo, eneo bunge la Nyando kwenye barabara kuu ya Kisumu – Nairobi asubuhi ya leo.

Inasemekana idadi ya waliojeruhiwa huenda ikaongezeka katika ajali hiyo iliyotokea majira ya saa nane na nusu alfariji ya jumatatu 29 januari mwaka 2024.

Kulingana na kamanda wa polisi wa kaunti ndogo ya Nyando, Grace Thuo dereva wa basi hilo alikiuka kanuni za trafiki ambapo alikuwa akipishana na gari lingine na hatimaye kusababisha ajali hiyo

Iliripotiwa kuwa basi lililokuwa likisafiri kuenda Nairobi kutoka mji wa Kampala lilipoteza mwelekeo na kugongana ana kwa ana na lori lililokuwa likiingia Kisumu.

Miongoni mwa waliofariki ni dereva wa basi pamoja na dereva wa Lori na Majeruhi wanatibiwa katika Hospitali ya rufaa ya Jaramogi Oginga Odinga wengine wakipelekwa katika hospitali ya Ahero.

Basi hilo linamilikiwa na kampuni ya usafiri wa mabasi ya Super Metro.

By Editorial desk