HabariNews

Wadau wa Vyuo Vikuu watakiwa kuainisha Kozi Kufanikisha Mtaala wa CBC

Waziri wa Elimu nchini Ezekiel Machogu ametoa wito kwa Machansela, wahadhiri wakuu wa vyuo vikuu na washikadau wengine katika sekta ya elimu kote nchini kuanza kudurusu upya mtaala wa Elimu ili kufanikisha mtaala wa Elimu ya umilisi almaarufu CBC.

Akizungumza mnamo Jumatatu katika ufunguzi wa warsha ya siku tano ya Wahadhiri wakuu wa vyuo vikuu iliyoandaliwa mjini Mombasa, Machogu aliwataka washikadau wa Elimu kuanza harakati za kudurusu mitaala yao ya masomo ili kurahisisha ufanisi wa Mfumo wa Elimu wa CBC.

Waziri huyo vile vile alitaka vyuo vikuu nchini kutoa mafunzo yatayowafaidi wanafunzi wanapohitimu huku akipendekeza masomo yasiyo na msingi kutolewa kwenye mtaala.

Waziri Machogu hakuchelea kuzungumzia suala la Ukosefu wa maadili na Ufisadi vyuo vikuu.

Aliifichua kuwa wizara yake itachukua hatua kali za ki sheria kwa wale wanapunja na kufuja rasilimali za umma vyuo vikuu.

Waziri huyo aliahidi kuwa Serikali kuu kupitia wizara yake ya elimu itaendelea kutoa ufadhili wa masomo kwa wanafunzi wa vyuo vikuu pasi kuchelewesha.

Aidha alisema kuwa Vyuo vikuu vya umma vitapokea mgao fedha wakati ufaao ili kufanikisha shughuli zote masomo katika vyuo vikuu.

Warsha hii ya siku tano na wahadhiri wakuu wa vyuo vya umma kote nchini inajiri huku madai yakibuuliwa ya kucheleweshwa kwa mgao wa ufadhili wa vyuo vikuu.

BY ISAIAH MUTHENGI