HabariLifestyleMazingiraMombasaNews

Mwanamume anayedaiwa Kumwua Mkewe na Kumjeruhi mtoto huko Kwale Ajisalimisha

Idara ya Polisi Kaunti ya Kwale imetangaza kujisalimisha kwa mshukiwa wa mauaji eneo la Samburu hii leo.

Mshukiwa huyo mwanamume mwenye umri wa makamu amehusishwa na mauaji ya mke wake mwenye umri wa miaka 25 na kisha kumjeruhi mwanawe wa mwaka mmoja kwa kumkata panga katika kijiji cha Julani A eneo la Mwavumbo.

Akithibitisha kisa hicho Mkuu wa Polisi wa Samburu Lydia Mambo amesema marehemu Pauline Mbeyu Kaingu amepatikana nyumbani mwake akiwa tayari ameshakufa huku mwili wake ukiwa majeraha makubwa mwilini na mikono yake ikiwa imekatwa.

Afisa huyo ametoa wito kwa wanandoa kutatua mizozo yao kwa amani na kuhakikisha wanadhibiti hasira zao.

Mwanamume huyo anatarajiwa kufikishwa mahakamani kufunguliwa na kujibu mashtaka ya tuhuma za mauaji.

Bad things happen in life.

Hata hivyo Chanzo cha mauaji hayo aidha hakijabainika huku kisa hicho kikijiri wiki moja tu baada ya kisa cha wanawake wawili waliokuwa wake wenza kuuwawa na jamaa mmoja eneo la Kinango katika Kaunti hiyo.

BY BINTIKHAMIS