HabariMakalaMombasaNewsSiasaWorld

Vuta ni kuvute ya uongozi katika baraza Kuu la waislamu SUPKEM

Vuta ni kuvute ya uongozi katika baraza Kuu la waislamu SUPKEM ilizidi kutokota huku wanachama wa baraza hilo kanda ya Pwani sasa wakimtaka aliyekuwa Mwenyekiti wa baraza hilo Yusuf Nzibo Kukoma kutoa madai ya kupotosha kwa umma kuhusu uongozi wa baraza hilo.

Wakiongozwa na Naibu mwenyekiti wa kitaifa SUPKEM Sheikh Muhdhar Khitamy viongozi hao waliitaka serikai kuingilia kati na kumkomesha msajili wa vyama kukoma kutatanisha uongozi wa SUPKEM kinyume cha maagizo ya mahakama.

Khitami alieleza kuwa afisi ya msajili iliendelea kusababisha mzozo kwa kumkabili aliyekuwa mwenyekiti wa baraza Yusuf Nzibo fomu ya “H” ya mwaka 2017 huku fomu inayotambuliwa ni ile ya mwaka 2023 ya uchaguzi wa baraza hio.

“Maneno ni yale yale, imekuwa ni kiriba gorji , gorji kiriba.Nzibo alitolewa miaka mitano iliyopita na wanachama wenyewe wa kenya nzima.Akapeleka kesi kortini na alipoona atashindwa akaiomba korti kwamba ataskizana na sisi na kusema hataki tena kesi.”alisema Khitamy

Kwa upande wake Mshirikishi wa SUPKEM Ukanda wa Pwani Hamisi Mwaguzo aliwasihi wanachama wa Baraza hilo kote nchini kuwa watulivu na kuacha sheria itumike.

Mwaguzo alidai Nzibo anapotoshwa na baadhi ya watu ambao pia si wanachama wa SUPKEM ili kuhujumu utendakazi wa baraza hilo kwa kuendeleza ufisadi jambo ambalo wameapa kamwe hawatakubali.

”Napenda kuwaambiwa wakubwa wote wa SUPKEM nchini wawe na utulivu kwa sababu ofisi ya kitaifa ina viongozi shupavu wanaojua sheria ivo basi wasitikiswe na kitu chochote.”Alisema Hamis Mwaguzo

Viongozi hao wa supkem walisema kuwa wataendelea kumtambua Hassan ole nado kama mwenyekiti hadi pale uchaguzi mwengine utakapofanyika huku wakieleza kuwa tayari waliwasilisha malalamishi yao mahakamani kumkomesha nzibo kutoa matamshi ya utata kuhusu uongozi wa supkem

“Nzibo,shirika na wafuasi wake sio wanachama wa SUPKEM kwa maana hana stakabadhi za kuwa mwanachama hivo basi hana budi kusalia kimya kwa maana tunamtambua Ole Nado kama mwenyekiti.”Aliongeza Khitamy

Haya yanajiri siku moja baada ya kundi moja linaloongozwa na aliyekuwa mwenyekiti wa baraza hilo Yusuf Nzibo kunyimwa idhini ya kuingia katika afisi za SUPKEM baada ya kushindwa kutoa stakabadhi sahihi za kumuoyesha kuwa yeye ndiye mwenyekiti.

BY NEWS DESK