HabariNews

Gharama ya Maisha Yasalia Kero Kwa Haki Za Kijamii

Gharama ya juu ya maisha na Mazingira magumu yametajwa kuwa changamoto kuu inayokabili masuala ya haki kwa jamii.

Afisa wa Dharura kutoka shirika la Haki Afrika Mathias Shipeta alisesema hali ngumu ya maisha imepelekea Wakenya wengi hasa watoto na wajane kutumika vibaya ili kujimudu kimaisha.

Aidha Shipeta alisema kuwa swala hilo litaweza kutatuliwa iwapo jamii italinda watu ambao wako na urahisi kupatwa na visa vya dhuluma kama vile wajane,wazee, watoto na akina mama wasio kuwa na waume .

“Gharama ya maisha imepanda,Wakenya wengi hawawezi kupata hata mlo mara mbili kwa siku,wajane watoto kina mama wako katika katika njia rahisi ya kudhulumoiwa wengine wanatumika vibaya ili wapewe pesa kwa hivyo swala la watoto sasa limekuwa zito,nyingi ya haki za kijamii zinaweza kutatuliwa iwapo jamii italinda wale watu ambao wako mstari wa mbele kupatwa na visa vya dhulma.“ Alisema Shipeta

Vile vile Shipeta alilitaja swala la upatikanaji wa huduma za mahakama kuwa miongoni mwa changamoto hizo akisema ongezeko la kesi mahakamani, rasilimali na muda wa kuendeleza kesi mahakamani zimelemaza shughuli hizo hali ambayo imepelekea mashirika ya kijamii kufungua vituo vya upatikanaji wa haki mashinani.

“Visa vya dhuluma wakenya wengi hawawezi kuenda mahakamani,kupata huduma za mahakama imekuwa ngumu muda pia hawana na rasilimali za kuendeleza kesi mahakamani sasa imebidi mashirika ya kutetea haki za bindamu kuja na vituo vya haki na changamoto kwetu ni kuwa kesi ni nyingi na tumezidiwa na inabidi serikali iingilie kati ili tuweze kupunguza kesi hizi.” Alisema Shipeta

Haya yanajiri huku ulimwengu ukiadhimisha siku ya haki za kijamii Kauli mbiu ya mwaka huu ikiwa ni Kuondoa Mianya, na Kujenga Miungano (Bridging Gaps, Building Alliances.)

BY MEDZA MDOE