HabariNews

Zaidi ya kampuni za bima 30 zitakongamana hapa Mombasa katika uwanja wa makadara

Zaidi ya kampuni za bima 30 zitakongamana hapa Mombasa katika uwanja wa makadara kutoa hamasa na mafunzo kuhusu bimba mbalimbali kwa wananchi.

Akizungumza katika kipindi cha gumzo pevu hapa sauti ya pwani Meneja wa Mamlaka ya Kudhibiti Mashirika ya Bima nchini IRA Evans Kibagendi alieleza haja ya wakaazi katika ukanda wa pwani kuhudhuria kongamano hilo ambalo litafanyika wiki hii kuanzia ijumaa tarehe 23 hadi jumamosi 24 Februari 2024.

Akikifafanua umuhimu wa bima kwa wahudumu wa bodaboda nchini Kibagendi ametaja wahudumu hao kuwa miongoni mwa watu walio kwenye hatari wakati wa kuendesha shughuli zao akieleza umuhimu wa wahudumu wote wa bodaboda kujisajili katika bima binafsi mbali na ile ya pikipiki zao.

Alibaini kuwa ili kuepukana na mahangaiko inapotokea ajali, kila boda boda anafaa kuwa na bima hiyo ambayo itamsaidia katika matibabu na malipo kwa familia endapo mmoja atafariki.

“Kulingana na maisha iyo bodaboda it’s very risky, because wale jamaa yjey are exposed to accidents and other risks. So they should also take kitu tunasema kama personal accident.

Personal accident ni product ya insurance unachukuwa unapoumia unaenda hospitali na hiyo card, unapoumia familia zako zinapata malipo,” alisema Kibagendi,” alisema Kibagendi.

Kibagendi alidokeza za kuwa mamlaka ya IRA imezindua mpango wa BIMA MASHINANI unaolenga kuhamasisha wananchi hasa bodaboda kuhusu umuhimu wa bima mbalimbali kote nchini.

“Bima mashinani tunataka kwenda kwa wananchi. Tumeenda kwa kila kaunti tunalete boda boda leaders kutoka sub- county, Ward up to the county level all leaders a hundred of them tuko na budget tunaenda tunawaweka kwa classroom, tunawapeleka tunawelezea umuhimu insurance mbalimbali.” Aliongeza Kibagendi.

Hata hivyo visa vya watu kulalamikia ulaghai katika kampuni za bima hapa nchini , Meneja huyo aliwaondolea shaka wakaazi wa pwani na taifa kwa jumla kwani mamlaka hiyo ina idara maalum ya kushughulikia dhuluma na lalama dhidi kampuni za bima zinazokiuka makubaliano na wateja wao.

“Nina kuhakikishia kuwa katika IRA tuko na idara moja, Department ambayo inaitwa consumer protection. Cosumer protection ni department ambae inatumukia wananchi…”

BY MAHMOOD MWANDUKA