HabariNews

SikuYaKimataifaYaWanawake2024: Jamii Yatakiwa kuwaunga mkono Wanawake na Kukomesha Dhulma

Ulimwengu ukiadhimisha siku ya kimataifa ya wanawake, jamii imehimizwa kuwaunga mkono wanawake na kutambua umuhimu wao katika jamii badala ya kuwabagua na kuwakandamiza.

Maadhimisho hayo yaliyoanza kuadhimishwa mnamo mwaka 1911, yanasemekana kuwa mbinu ya kuihamasisha jamii kutambua umuhimu wa wanawake katika jamii.

Kwa mujibu wa Linda Shuma mwanaharakati wa maswala ya jamii katika shirika la Women and Girls Empowerment mjini Kilifi, juhudi nyingi za kuwawezesha wanawake zinalenga kumkwamua kutokana na ukandamizaji uliopo kwenye mila na itikadi za jamii.

Amekanusha madai kuwa sheria nyingi zimeundwa kumlinda mwanamke na kukosa kumuangazia mwanamume, akisistiza kuwa sheria hizo nizakuleta usawa katika jamii kati ya wanawake na wanaume.

Ikumbukwe rais William Ruto anatarajiwa kuliongoza taifa katika maadhimisho hayo katika kaunti ya Embu. Kauli mbiu ya maadhimisho hayo yanayofanyika kila tarehe nane machi, ni wekeza kwa wanawake harakisha maendeleo.

BY ERICKSON KADZEHA