HabariNews

Taifa Liko Imara Katika Vita Dhidi Ya Pombe Haramu

Naibu Msemaji wa serikali Mwanaisha Chidzuga amesema serikali inafanya juhudi zote kuhakikisha inakuwa mstari wa mbele katika vita dhidhi ya pombe haramu.

Chidzuga alisema hatua ya serikali kufunga maeneo ya kuuza pombe ni katika juhudi za kuhakikisha biashara hiyo inafuata sheria bali sio kuharibu.

Aidha Chidzuga alisisitiza kuwa kama taifa ni sharti lihakikisha vita dhidhi ya pombe haramu vinasitishwa akiongeza kuwa maafisa wa usalama wanaohusika na biashara haramu ya pombe watakabiliwa na mkono wa sheria.

“Ukiangalia athari za pombe haramu na dawa za kulevya hapa nchini ukilinganisha na faida hivyo viwili haviwezi kufanyika ,hatufugi kuharibu baishara tunafunga tukifuata mikakati iliyowekwa iwapo unataka kufungua biashara yako fuata,tunasema iwapo unataka kufungua baa yako hakikisha zinafuata sheria” Alisema Chidzuga

Kuhusiana na maswala ya unyakuzi wa ardhi Pwani Chidzuga alidokeza kuwa ukosefu wa ufahamu kuhusu umiliki wa ardhi miongoni mwa wakaazi kuwa changamoto kuwa akisema kwa sasa wakaazi wameelimishwa kuhusiana na sheria hizo.

“wakaazi wengi wa Pwani tulikuwa hatuna ufahamu wa sheria za umiliki wa ardhi na wazee wengi walikuwa hawana hatimiliki kwa sababu zilikuwa zinamilikiwa na jamii, kwa sasa kuna mwangaza maana serikali imejitolea kuhakikisha tunahakikisha watua wanaelimishwa na wale ambao wananyakua ardhi serikali imeweza kuingilia kuhakikisha kwamba wanachukuliwa hatua.” Alisema Chudzuga.

BY MEDZA MDOE