HabariNews

Viongozi wa dini washabikia marufuku ya muguka Mombasa

Viongozi wa kidini kaunti ya Mombasa wameendelea kushabikia hatua ya serikali ya kaunti ya Mombasa kupiga marufuku muguka.

Katibu mratibu katika baraza la maimamu na wahubiri nchini CIPK Sheikh Mahmoud Abdillahi CIPK alisema marufuku hiyo imekuja kwa wakati kwani mugokaa umeharibu vijana wengi.

Kulingana na sheikh Mahmoud, huenda agizo hilo likaambatana na kashfa kutoka pande tofauti akimtaka gavana Nassir kuwa na kutoyumbishwa na mtu yeyote.

 “Tunamshukuru Mwenyezi Mungu kuweza kumpa fahamu kama hiyo ya kumpa uwezo na ujasiri wa kupiga marufuku jambo kama hili na sisemi kuwa hayatoliwa kwani madawa ya kulevya yalipigwa marufuku na bado watu wanauza na kula lakini yeye kama kiongozi amechukuwa maamrisho ya mtume Muhammad kwani amefikiria dini na akafikiria ubinadamu wa kukataza dawa za kulevya,” alisema Sheikh Mahmood.

Vilevile kiongozi huyo alimtaka gavana kuhakikisha mikakati imewekwa kwa asasi mbalimbali na maafisa wa serikali ya kaunti kukomesha ufisadi ambao utayumbisha vita dhidi ya zao hilo Mombasa.

Aliwataka viongozi wote wa kaunti ikiwemo wawakilishi wa wadi kushirikiana naye ili kufanikisha suala hilo.

“Gavana wetu asijione kama yuko pekeake, tuko pamoja nayeye na tunaomba wale viongozi wengine wamuunge mkono kuanzia MCA, wabunge na maseneta na wale ambao hawako ktika mrengo ambao gavana wetu yuko pia wamuunge mkono ili asijione kama yuko pekeake, vyovyote atakavyopelekwa sisi tuko na yeye.” Alisisitiza Mahmoud.

BY EDITORIAL DESK

Read alsohttp://sautiyapwanifm.com/2024/05/24/9958/