HabariNews

Serikali Yaimarisha Mikakati Ya Kufungua Bandari Eneo La Dongo Kundu, Mombasa  Hivi Karibuni

Mikakati ya kufunguliwa kwa bandari kwenye eneo la kiuchumi la Dongo Kundu kaunti ya Mombasa imefikia hatua nzuri, haya ni kulingana na Naibu mwenyekiti wa kitaifa wa chama tawala cha UDA Hassan Omar Sarai.

Akizungumza kwenye mkutano wa maandalizi ya chaguzi za mashinani za chama hicho  mnamo 6 Juni 2024, Sarai ambaye pia ni mbunge katika bunge la Afrika Masharika EALA alieleza kwamba wakaazi katika kaunti ya mombasa ikiwemo vijana na kina mama watapata afueni kwani watatengewa nafasi za ajira.

Kulingana na Sari mradi huo wa Bandari eneo hilo ambao unatarajiwa kuanzishwa hivi karibuni na serikali ya Kenya Kwanza  sio tu utakuwa kitega uchumi kwa taifa bali pia utawawezesha wakaazi wa eneo hilo kujikimu kimaisha.

 “DK1, Dongo Kundu one, na kutajengwa bandari mpya. Tumefika mbali sana katika kutoa kandarasi na sisi sio kujenga tu ambayo tunataka infrastructure tutahakikisha tukiwa tumeshikana na viongozi wengine wa UDA kwamba kila mkenya, wakaazi wa Changamwe, wakaazi wa Jomvu, wakaazi wa Mombasa watakuwa wa kwanza kupata ajira.

Katika hizi kazi pia tunaangazia kwamba vijana wengi zaidi kina mama na wengine kutoka hapa maeneo ya Mombasa West na maeneo ya Mombasa wapate fursa ya kwanza kupata ajira.” Alisema Sarai.

Wakati uo huo aliusifia mradi wa ujenzi wa nyumba za bei nafuu nchini akiutaja kama suluhu ya kuwainua wananchi wenye mapato ya chini.

Alidokeza kwamba serikali inalenga kuendeleza ujenzi wa nyumba hizo katika eneo Bunge la Changamwe, na Nyali ambapo zaidi ya wakaazi takriban 8,000 na 3,000 mtawalia wanatarajiwa kunufaika na mradi huo kwa kupata ajira na makaazi bora ya kuishi.

Kwa mujibu wa kiongozi huyo mradi huo utaleta usawa katika jamii kwani wakaazi wa eneo hilo wapatao elfu nane watapata makazi bora ya kuishi.

 “Kuna mipangilio katika katiba ya Kenya inaitwa social justice, usawa wa kijamii. Yule ambaye mwenye kidogo asaidiwe nay eye pia aimarike kabla ya yule mwenye kingi kuwa tajiri.

Tuko na hii affordabable housing program. Hii ni kuleta usawa wa jamii yule alioko juu ambebe kwa idadi kubwa yule alioko chini na yule alieko chini ainuliwe kw akupitia huduma za serikali”  aliongeza.

Akihimiza umuhimu wa kuwawezesha vija Sarai alidokeza mipango ya kuzindulliwa kwa vituo vya kukuza vipaji na sanaa katika maeneo bunge yote kaunti ya Mombasa.

Aliwataka viongozi katika kaunti ya mombasa kuwekeza pakubwa miradi itakayowafaidi vijana wasio na ajira ili kupunguza visa vya uhalifu na matumiz ya dawa za kulevya.

 “ Tunatengeza youth centres kukiwa na Changamwe youth Centre, Jomvu Youth Centre, Likoni Youth Centre na nyingine, pale ndio watoto wanaenda kushowcase talent zao kila weekend. Akishamaliza kusoma hawa vijana wetu wapatiwe fursa ya kuweza kuwatumbuiza”  alisisitiza Kiongozi huyo.

BY MAHMOOD MWANDUKA