HabariMombasaNewsSiasa

Rais Ruto Apata ‘Watetezi’ wapya Pwani; Viongozi Waimba na Kuhubiri Ajenda za Serikali

Viongozi mbali mbali wa Mombasa na Pwani wameendelea kupigia debe na kuuunga mkono ajenda za serikali Jumuishi ya rais William Ruto.

Wakiongozwa na Gavana wa Mombasa Abdulswamad Shariff Nassir ambaye amempongeza rais Rutio kwa kuchukua jukumu la kuwaleta viongozi mbalimbvali pamoja na kuweka kando tofauti za kisiasa na kikabila ili kuunda seriakli moja kwa manufaa ya wananchi.

Akizungumza katika eneo bunge la Likoni wakati wa ufunguzi wa chuo cha kiufundi cha Likoni gavana Nassir alimkosoa vikali aliyekuwa naibu wa rais Rigathi Gachagua kwa kile alichiotaja kama kuendeleza siasa mbovu na ukabila, akimtaja Gachagua kama ‘mwendawazimu’ anayestahiki kwenda kituo cha afya ya akili.

 “Yule anayeleta ukabila Kenya hii ni mwendawazimu aliye na malengo binafsi na anastahiki kwenda kituo cha afya ya akili, acha niseme ukweli, nitazungumza yaliyopo. Leo tunaambiwa mambo ya yule Chief Justice, kwani CJ ni wa Meru na waEmbu peke yake? Jaji Mkuu ni Wakenya wote, kabila zote, dini zote na rangi zote. Usihujumu mtu kwa malengo yako binafsi.” Alifoka Nassir.

Naye waziri wa michezo na masuala ya Vijana Salim Mvurya amemsihi rais kluendelea na utendakazio na kuwapa kisogo mahasidi wote wa serikali akiahidi kwamba viongozi wa ukanda wa pwani wanaunga mkono serikali iyake jumuishi mia fil mia.

Sisi tunaunga mkono wakati wewe unatengeza serikali ya kujumuisha ya kila mtu, na itaweza kuleta uthabithi maendeleo na uchumi.

Na wewe rais ulichaguliwa na Wakenya hakuna mwengine yeyote anaweza kukukataza kuzuru eneo lingine la Kenya na tunakemea hiyo kauli ambayo mwengine (Rigathi Gachagua) anasema ati Rais asikanyage kwingine, rais kanyaga Kenya na tutakuunga mkono.” Akasema Mvurya.

Kwa upande wake mbunge wa Likoni Mishi Juma Mboko alisifia nafasi mbalimbali serikalini walizopewa baadhi ya viongozi wa ODM, akitaja kuwa fursa nzuri kwao na wapwani kuunga mkono serikali.

Mishi alidokeza kuwa upande wao wa chama cha ODM utapata teuzi zaidi serikalini.

Wakati wa Ruto tumepata wizara, tumepata Hassan Joho, tumepata John Mbadi, Opiyo Wandayi, Attorney General na sasa tutapata makatibu wa kudumu ambao wataekwa na serikali ya William Ruto. Jamani anayekunyegeza mnyegeze na kama Ruto amefanya na unaendelea kutenda sisi tunakubali mambo yako.” Akasema Mishi.

Ni kauli iliyoungwa mkono na Mbunge wa Jomvu Badi Twalib Badi aliyezungumza huko eneo la Changamwe akisema kuwa watamuunga mkono Rais Ruto kuchaguliwa tena 2027, kwa kusimama na kinara wao Odinga na kushughulikia matatizo ya Wapwanii.

Barabara tumepata Changamwe, Jomvu tumepata na hata ziko nyingi, lakini jambo muhimu hawa vijana wetu wanahitaji ajira ili waishi kama wengine.

Na tutakuunga mkono rais tutafanya kazi na wewe, 2027 ni kumi bila breki.” Alisema.

Kauli zao zinajiri huku Kinara wa ODM aliyekuwa Waziri mkuu Raila Odinga akiahidi kutangaza mwelekeo wake wa kisiasa hivi karibuni baada ya kufeli kunyakua nafasi ya Uenyekiti wa kiti cha AUC.

Hatua itakayotangazwa na Odinga hata hivyo inatabiriwa kuwa itakuwa ya kuunga mkono serikali, na kuigeuza Pwani ambayo muda mrefu imesalia upinzani na kuwa ngome kuu ya Odinga katika chaguzi kuu zilizopita.

By Mjomba Rashid