HabariNews

Mchanganuzi wa masuala ya uongozi Hassan Albeit ahimiza Uhusishwaji wa uma kuhusu mfumo wa ONE-MAN-ONE-SHILLING-ONE-VOTE

Mchanganuzi wa masuala ya uongozi na siasa ukanda wa Pwani Hassan Albeit ameeleza haja ya wananchi kuhamasishwa kuhusu  mfumo wa ugavi wa mapato kwa kuzingatia idadi ya watu one-man-one-vote-one-shilling.

Akizungumzia mjadala huo Jumanne ya 11 Juni 2024, ambao umedumu kwa zaidi ya wiki tatu sasa, Albeit ambaye pia ni Kaimu Kiongozi wa Chama cha PAA alibaini kwamba hata iwapo mswada kuhusu suala hilo utawasilishwa katika bunge la seneti na lile la Kitaifa huenda ukakosa tija kutokana na utendakazi wa mabunge ambayo mara nyingi hutumia idadi ya wabunge kupitisha ajenda fulani.

Albeit alisema suala hilo halifai kuharakishwa kwani kuna mambo mengi ambayo yanafaa kuangaziwa kabla ya kupata mwelekeo unaofaa.

“hawa ambao leo tunafikiri watatuwakilisha hawa wana tyranny of number, kuna tyranny of number katika seneti kuna tyranny of  number katika parliament. Wakitumia hii tyranny of number kutakuwa kumepatikana uadilifu? Justice itakuwa imepatikana?

Kwa hivyo the best way ni irudi katika public participation we start afresh na watu mwanzo waelimishwe kabla hawajaparticipate katika public participation…”Alisema Albeit.

Aliongeza kuwa mjadala huo umetokana na mfumo wa demokrasia ambao unatumika nchini akisema mfumo huo umefeli akiutaja kama moja ya sababu ya changamoto katika taifa la Kenya kama vile maendeleo kuelekezwa sehemu moja.

“Concern ya hawa wanasema ya kwamba funds zinazotolewa haziwabenefit  zaidi sababu hao ni wengi ama ni kidogo kuliko chakula wanachopewa  na sisi tunacomplain kwamba maendeleo yetu ni kidogo na tumekaa hivyo kwa muda mrefu sana sasa hapo kuna mambo population watu kuwa wengi,  kuna mambo ya marginalization ambayo imeweza kufanyika kwa muda mrefu.

Sasa hii yote tatizo kubwa hili yaja na hii democracy, kwa sababu democracy is a failed system kwa sababu hii one man one voteone shilling inakuja na formulae ya tyranny of numbers,” aliendelea kueleza.

Akiutaja mfumo huo kama utakaoleta mgawanyiko wa kibaguzi mkubwa nchini, Mchanganuzi huyo alieleza haja ya mfumo maalum kuwekwa ili pande zote zipate kuangaziwa.

Kadhalika ili kufanikisha mendeleo katika maeneo yote katika jamhuri ya Kenya, Albeit  alitoa changamoto kwa uongozi hasa wa kitaifa kuhakikisha maendeleo katika maeneo yanazingatia uwezo wake badala ya idadi ya watu wanaopatikana.

“Democracy ilipelekea development mahali pamoja , ntakupa mfano mfupi tu, mahali pazuri pa kulima sukari ni Tana River lakini ikapelekwa western Kenya 1963 kwa sababu ya Masinde Muliro kwa sababu ya kutakia watu wake  maendelo ikabidi apeleke kule .

Si lazima kila mahali kuwa na watu wengi lakini tuangalie kwazalisha nini  kama Tana River kwaeza kuwa ni mahali pa mazao ya kusaidia kenya kwa hivyo we should be thinking kwamba yaani ati kwa sababu ni mwitu mkubwa msifanye development, leo North Eastern kukifanywa proper research kwaeza kuzalisha,” alisisitiza Albeit.

Hata hivyo kundi la viongozi kutoka maeneo yenye ukubwa wa kieneo na idadi ndogo ya watu hasa kaunti za mkoa wa Kaskazini Mashariki, Ukambani na Ukanda wa Pwani walipinga vikali mfumo huo wengine wakipendekeza mfumo wa ugavi utakaozingatia ukubwa wa kieneo, wengine wakisema kuna haja kurudi katika mfumo wa Majimbo ili kila wakaazi kutoka eneo fulani wanufaike kikamilifu na rasilimali zinazopatikana.

“Nataka tuelimishe watu wetu wajue kwamba hiyo ikifanyika, mgao wa pesa ambazo zinakuja kaunti  yetu ya Makueni itapoteza milioni 658, itakuwa ni minus. Hivi tunavyoongea leo ni  kwamba kuna constituency ambazo zina watu wengi ndio,  lakini ukiangalia mambo ya stima wako na 100 % electricity ,primary school zote ziko na electricity ,kila boma iko na electricity  sasa ukisema wale ambao ni wengi waongezewe pesa wakiongezewa pesa ya stima wataenda kueka wapi ama wataeka stima kwa choo.” Alisema naibu gavana kaunti ya Machakos Francic Maliti.

Mjadala huo ulianza kupamba moto wiki kadhaa zilizopita baada ya naibu wa rais Rigathi Gachagua kutangaza kuunga mkono mfumo huo, ambao pia ulikuwa katika mswada wa BBI.

Miongoni mwa viongozi waliounga mkono mfumo huo ni pamoja na kinara wa ODM Raila Odinga na viongozi kutoa eneo la Mlima Kenya.

Hata hivyo, rais William Ruto amesalia kimya kuhusu suala hilo ikisubiriwa iwapo atazungumza na kutangaza msimamo wake na vile vile iwapo mswada utawasilishwa katika bunge la seneti na lile la kitaifa kuhusu mfumo huo.

BY MAHMOOD MWANDUKA