Idara ya elimu eneo la Kauma kaunti ya Kilifi imewakikishia watahiniwa wa mtihani wa kitaifa kuwa wataendelea na mtihani wao bila tatizo lolote hata iwapo kutashuhudiwa mvua.
Mkurugenzi wa elimu kaunti ndogo ya Ganze Harry Odeche amesema serikali imeweka mikakati kabambe kuhakikisha hakuna mtahiniwa atakosa kufanya mtihani wake.
Kauli ya mkurugenzi huyu imejiri baada ya kubainika shule nyingi eneo hilo huathirika wakati wa mvua kutokana na uwepo wa mito karibu na shule.
Mkurugenzi huyo wa elimu amesema kuwa tayari mipango ya kuwahamisha watahiniwa hadi shule zingine eneo hilo imewekwa.
Wakati Huo huo mkurugenzi huyo amesema watahitaji magari ambayo yatakabiliana na mvua ili kusambaza mitihani katika maeneo hayo telezi, mvua itakapoanzo.
Aidha Odeche amesema eneo hilo lina vituo 19 vya watahiniwa wa mitihani ya shule za msingi pamoja na vituo 4 vya mitihani ya shule za upili.
By Aisha Juma