Viongozi wa dini pamoja na waumini wa dini ya kiislamu Lamu wanasema hawajaridhishwa na hatua ya rais Uhuru Kenyatta kuongeza muda wa kafyu kwa siku 60 wakidi itatatiza shughuli za mwezi mtukufu wa ramadhan.
Wakiongozwa na mwenyekiti wa bazara la viongozi wa dini mbali mbali Mohamed Abdulkadir, wanasema walitarajia rasi Kenyatta kutangaza masharti ambayo hayatakinzana na maadhimisho ya mwezi huo.
Abdulkadir amesema huenda ikawa vigumu kwao kuhudhuria swala za usiku na alfajiri ikizingatiwa maombi hayo hufanyika nyakati za kafyu.
Ustadh Mohamed Mahfudh anapendekeza kiongozi wa taifa angeweka mda wa kafyu kuanzia saa tano usiku hadi saa kumi alfajiri.
Wakati huo huo wamepongeza hatua ya rais kupiga marufuku mikusanyiko ya watu pamoja na ya kisiasa kwa siku thelathini, wakisema italeta utulivu miongoni mwa wanaokiuka masharti ya kukabili maambukizi ya virusi vya corona.
By Joseph jira