Tume ya maadili na kupambana na ufisadi nchini EACC imedai kwamba ufisadi bado umekithiri na kulamaza shughuli nyingi nchini licha ya juhudi za tume hiyo za kukabiliana na ufisadi.
Tume hiyo inasema kuwa kwa miaka mitano iliyopita imeweza kufichua visa vya ufisadi vya takribani shilingi bilioni 30.4.
Kulingana na naibu msimamizi wa masomo katika tume hiyo Gilbert Lukhoba, kesi 1000 za ufisadi zimekamilika mwaka huu, huku kwa miaka mitano, mali yenye thamani ya shilingi bilioni 25 ikitwaliwa na serikali.
Lukhoba ambaye alikuwa amuhudhuria hafla ya masomo kwa waandishi wa habari ameongeza kuwa ipo haja ya waandishi wa habari kujitolea katika kupigana na janga hili la ufisadi ambapo taifa la Kenya limekuwa likinakili visa vingi vya ufisadi.
Hata hivyo kulingana na Lukhoba kufikia sasa tume hiyo imeweza kupiga msasa mitandao 15 ya idara tofauti nchini pamoja na kaunti 20.
Lukhano ametoa wito kwa wananchi kushirikiana na tume hiyo kwa kujitolea kutoa habari muhimu kuhusu visa vya ufisadi
By Joyce Mwendwa.