Rais Uhuru Keyatta amesisitiza umuhimu wa BBI na harsara ambayo itakumba wakenya kutokana na maamuzi mabovu ya mahakama kuhusu BBI.
akihutubia wakenya wakati maadhimisho ya sikuku ya Madaraka katika uwanja wa kimataifa wa Jomo Kenyatta, Rais Kenyatta amesema wakenya watapoteza mabilioni ya fedh iwapo mapendekelzo ya bbi bhayatatekelezwa kutokana na maamuzi ya kibinafsi ya mahakama.
Kenyatta aidha amesema kuwa katika utawala wake serikali imefanya bidii kuhakisha kwamba taifa la limesonga mbelie likiunganishwa na serikali za awali.
hatahivyo hakusita amempongeza kinara wa ODM Raila Odinga kwa ushiriano wake na serikali kupitia salamu za heri maarufu handshake pasi na kujali maslahi yake binafsi.
Tangu kutengana kwa rais Uhuru Kenyatta na naibu wake William Ruto,akenya wengi walingoja sana kumuona naibu wa Ruto wakati wa hafla iliyotendeka katika uwanaja wa Jomo Kenyatta Kisumu.
Hotuba yake naibu rais ilisubiriwa sana na wakenya, kwani kumekuwa na mgogoro kati ya vigogo hao wawili.
hatahivyo Ruto alioekana kuipongeza juhudi za rais Uhuru Kenyatta na serikali ya jubilee kwa kuendeleza miradi ya maendelleo bila kujali eneo wala kabila.
Wakati huohuo Raila Odinga aliwakumbusha wakenya jinsi viongozi waliotagulia walivyoshirikiana na kuweka siasa zao kando ili kuweza kuleta wakenya pamoja katika siku kama hizi za kitaifa.