Katibu mkuu wa muungano wa wahudumu na wamiliki wa tuktuk kaunti ya Mombasa Jacob mwendwa amewahimiza wahudumu wa tuktuk kutokuwa na wasiwasi kuhusu stakabadhi wanazoitishwa ili kukata cheti maalum cha usalama.
Akizungumza na wanahabari Mwendwa amesema serikali ya kaunti ya Mombasa inaendeleza zoezi hilo bila malipo na malipo pekee yanayohitajika ni shilling mia tano ya kuchapisha cheti hicho.
Aidha Mwendwa amewahakikishia wahudumu hao kuwa stakabadhi zao ziko salama kwani hakuna mtu anaweza kuzitumia kwa njia isiyofaa.
Kwa upande wake mwenyekiti wa wahudumu wa Tutkuk katika eneo la kongowea Martin Kelly amewataka wahudumu wote kujisajili na kupata cheti hicho kwa minajili ya usalama wa abiria.
Awali wahudumu hao walikuwa wamedinda kutoa stakabadhi zao wakihofia usalama wa biashara zao.
By Warda Ahmed