Waziri wa leba nchini Simon Chelugui amesisistiza kwamba serikali kwa sasa haina uwezo wa kuongeza mishahara na marurupu katika kipindi cha miaka miwili kutokana na upungufu mkubwa katika hazina ya fedha baada ya janga la korona kulemeza shughuli muhimu humu nchini.
Akizungumza na wandishi wa habari katika kongamano lilioleta pamoja wasimimiza wa masuala ya ajira nchini IHR katika hoteli ya Sarova Mombasa, waziri wa leba Chelugui amesema kuwa itakuwa ni jambo ngumu kwa serikali kuweza kuwaongezea mishahara na marupurupu wafanyikazi wa serikali hasa nyakati hizi za janga la korona.
Aidha ameongeza kuwa serikali inamipango dhabiti ya kuwahakikishia wakenya ambao kwa sasa wamehitimu katika idara mabli mbali na hawana ajira, kwamba wanapata ajira katika mataifa ya nje ili kusaidia katika ukuaji wa uchumi na kupunguza kesi za ukosefu wa ajira nchini.
Waziri chelugui amesema hayo katika kongamano la 7 la maaafisa wa kusimamia ajira na maslahai ya wafanyikazi ambalo huandaliwa kila mwaka.
BY DAVID OTIENO