Serikali imepanga kupanua uwezo wa kuhifadhi damu kutoka panti 20,500 hadi panti 49,500 kufika mwisho wa mwezi huu.
Vyumba vitatu vya baridi katika benki za mkoa kwa sasa ziko katika ukarabati kama njia moja ya kukaba upungufu wa damu nchini ,ambayo imeona kuongezeka kwa kasi rufaa za mchango wa damu.
Wizara ya afya imetoa vyumba vitatu baridi vya kuhifadhi damu vilevile majokofu 8 hatua ambayo inatarajiwa kuenda mbali katika kuhakikisha kuwa hakuna mgonjwa yeyote atakaye kosa damu nchini.
Waziri wa afya Mutahi Kagwe amehimiza kaunti zisizo na taasisi za damu kuanzisha kwa masaada kutoka huduma za kitaifa za kuhifadhi damu.
BY NATASHA SAGHE