Naibu wa rais William Ruto amewashutumu vikali wapinzani wake wanaochulia kwa mzaha kauli mbiu ya Wheelbarrow na mfumo wa bottom up economic model bila ya kujua malengo yake.
Ruto anasema baadhi ya wapinzani wake wanafanya makusudi na kukashifu na kudunisha wheelbarrow bila kujua inaashiria mageuzi makubwa yatakayofanikishwa kupitia mfumo wa bottom up economic model mfumo wa kiuchumi unaowalenga wakenya wa matabaka ya chini.
Ruto aidha amefafanua kwamba wheelbarrow ni kifaa cha msingi cha kufanyia kazi.
Kwenye kikao na viongozi wa kisiasa pamoja na wa kidini wa kaunti Makueni nyumbani kwake huko Karen, naibu wa rais amewataka wapinzani wake kuwaeleza wakenya maana ya nembo za vyama vyao kwa mfano nembo ya chungwa katika chama cha ODM.
Wakati huo huo Ruto amesema wakenya wamepoteza imani katika upinzani.
Kulingana na Ruto upinzani ulikuwa na wakati bora kuishinikiza serikali kutekeleza ajenda za maendeleo ila umedhihirisha kwamba hauna uwezo huo.
Mfumo wa bottom up economic model umekuwa ukikosolewa na wapinzani wa Ruto.
By Warda Ahmed