Rais Uhuru Kenyatta amefanya mabadiliko ya Baraza lake la Mawaziri.
Katika mabadiliko yaliyotangazwa na msemaji wa Ikulu ya Rais Bi Kanze Dena, Charles Keter ambaye alikuwa waziri wa Kawi sasa amepelekwa katika wizara ya Ugatuzi, Monicah Juma aliyekuwa katika Wizara ya Ulinzi amepelekwa katika Wizara ya Kawi huku Eugine Wamalwa aliyekuwa katika wizara ya Ugatuzi akihamishwa hadi katika wizara ya ulinzi.
Wakati huohuo rais pia amefanyia mabadiliko makatibu wanne kutoka wizara mbalimbali,pamoja na ubadilishaji wa majina ya baadhi ya idara za serikali.
Mabadiliko hayo yanatarajiwa kuanza mara moja.
Rais Uhuru Kenyatta ameagiza Wizara ya Nishati kutekeleza mabadiliko ya kupunguza gharama katika Kampuni ya Umeme kenya power (KPLC).
Kenyatta amekubali jopo kazi lilioundwa Machi 2021, kuanzisha mchakato wa kupunguza gharama ya umeme kwa asilimia 33.
Mapendekezo mengine na jopo kazi hilo ,ni kujadiliana na wazalishaji wa umeme wa kujitegemea (IPPS) ili kukatwa ushuru wa haraka wa mikataba ya ununuzi wa nguvu (PPA) katika mipango ya mikataba iliyopo.
BY NEWS DESK