Afya

Shughuli ya kutoa chanjo ya Corona kwa vijana wa umri wa miaka 15 hadi 18 yaanza.

Wizara ya afya imeanza rasmi shughuli ya kutoa chanjo dhidi ya virusi vya Corona kwa vijana wa umri wa miaka 15 hadi 18 licha ya shiririka la afya duniani WHO kushauri kuanzia vijana wa miaka 12 hadi 18.
WHO iliorordhesha aina ya chanjo hizo na umri wa watu wanaopaswa kuchanjwa kama vile chanjo ya Johnson & Johnson, Pfizer mna Moderna hazipaswi kutolewa kwa watu wenye umri wa chini ya miaka 4.
Aidha chanjo ya Pfizer inaruhusiwa kutolewa kwa watu wenye umri wa miaka 5 hadi 11 huku chanjo zingine zikiwa haziruhusiwi.