Habari

MASHIRIKA YA KIJAMII YAWATAKA WAKENYA KUTOKAA KIMYA KUFUATILIA KUPANDA KWA BIDHAA KILA UCHAO.

Shirika la kutetea haki zakibinadamu la Haki Afrika limewataka wananchi wa kenya kutokaa kimya kufuatilia kupanda kwa bidhaa kila uchao.
Kauli hii inajiri baada ya mafuta ya petroli,diseli na mafuta ya taa kupanda kwa shilingi 9 mtawalia ambapo hali hii itapelekea bidhaa nyengine kupanda bei zaidi nakufanya maisha ya mwanchi kuwa ya ghali.Hussein Khalid ni mkurugenzi mkuu wa shirika la Haki Afrika.
Hatahivyo shirika hilo sasa limemtaka mwanchi kujitoa kimasomaso ili kupigania rasili mali ya Kenya ili kwa manufaaa yao.

>> News Desk…