Waziri mteule wa wizara ya usalama wa ndani ya nchi Profesa Kindiki kithure amesema sheria lazima ifuatwe bila kujali kabila wala cheo cha mtu anayefanya makosa nchini.
Kindiki ameyasema haya, mapema leo mbele ya kamati ya bunge inayopiga msasa mawaziri walioteuliwa na Rais William ruto.
Ameongeza kuwa eneo la kazkazini mwa kenya pia linafaa kupewa kipaumbele na kuhakikisha kwamba wananchi wanashirikishwa vilivyo na serikali katika kuleta amani.
Vilevile amesema kuwa atashinikiza utumiaji wa teknolojia zaidi katika kuwakabili wanaohusika katika kufanikisha makosa ya trafiki.
Kithure amewaka wazi thamani ya utajiri wake ikiwa ni shilingi milioni 544.
Kwa sasa Waziri mteule wa fedha prof. Njuguna Ndung’u anaendelea kuhojiwa akisema kuwa thamani ya utajiri wake ni shilingi milioni 950.
BY EDITORIAL DESK