HabariNewsSiasa

CIPK YAMTAKA RAIS WILLIAM RUTO KUANZISHA UCHUNGUZI KUBAINI WALIKO MAMIA YA WAKENYA WALIOPOTEZWA KIKOSI CHA SSU.

Baraza la maimamu na wahubiri nchini CIPK Sasa linamuomba rais William Ruto kuanzisha uchunguzi kubaini waliko mamia ya wakenya waliopotezwa na washukiwa wanaodaiwa kuwa polisi.

Kwenye kikao na wanahabari hapa Mombasa baraza hilo likiongozwa na Sheikh Mohamed Dor, limepongeza hatua ya kuvunjwa kwa kikosi cha Special service unit SSU wakisema majukumu ya polisi ni kuwalinda wananchi na wala sio kuwapoteza.

Wakati huo huo baraza hilo limepongeza kuteuliwa kwa Mohamed Amin kuongoza kitengo cha ujasusi DCI na kumuomba kutumia ujuzi wake kutegua kitendawili hicho.

BY EDITORIAL TEAM