Shirika la msalaba mwekundu nchini limesema kuwa watu million 6.4 watakabiliwa na baa la njaa ifikapo mwezi Januari mwakani ilikinganishwa na watu million 5.1 ambao wanakodolea macho janga hilo kwa sasa.
Shirika hilo likisema kuwa ni sharti hatua za haraka zichukuliwe kukabili hali hiyo .
Akizungumza katika eneo la Diani kaunti ya Kwale wakati wa hafla ya kuchangisha fedha kuwasaidia waathiriwa wa baa la njaa katibu mkuu wa shirika la msalaba mwekundu Dr. Asha Mohamed amesema kuwa licha ya mvua zinazoshuhudiwa katika sehemu mbali mbali nchini kwa sasa hata hivyo hazitoshi.
Akisema kuwa kutashuhudiwa afueni ya muda kutokana na mvua hivyo japo si kila mahali mvua hiyo imenyesha.
Katibu huyo ameongeza kuwa kaunti ya Kwale ni miongoni mwa kaunti hatari zaidi zilizoathirika na baa hilo la njaa.
kwa upande wake gavana wa Kwale Fatuma Achani amesema kuwa wanamipango ya kujenga mabwawa makubwa zaidi baada ya mabwana 723 yanakaribia kukauka kutokana na kiangazi cha muda mrefu.
BY EDITORIAL TEAM