Idara ya usalama kaunti ya Kwale imetakiwa kutilia mkazo marufuku ya sherehe za usiku zikitajwa kuchangia pakubwa visa vya mimba na ndoa za mapema katika jamii.
Haya ni kulingana na gavana wa Kwale Fatuma Achani akizungumza huko Vigurungani, eneo bunge la Kinango, ameihimiza jamii iiunge mkono hatua hiyo.
Kwa upande wake Kamishna wa Kaunti ya Kwale Gideon Oyagi amekariri kuwa vyombo vya usalama vipo macho na kamwe havitaruhusu sherehe za harusi au disco matanga nyakati za usiku.
Kauli za viongozi hao zimeibuliwa na shinikizo za mmoja wa viongozi kutaka sherehe hizo ziruhusiwe tena akidai zinawanyima riziki baadhi ya vijana (DJs) wanaotegemea sherehe hizo kama ajira.
BY EDITORIAL DESK