HabariNews

Huenda sekta ya utalii kaunti ya Kwale ikaimarika siku zijazo.

Huenda sekta ya utalii kaunti ya Kwale ikaimarika siku zijazo baada ya serikali kupitia shirika la kuhifadhi wanyamapori KWS kuahidi kuleta wanyama katika mbuga ya Mwaluganje.

Mkurugenzi wa Shirika la kuhifadhi mazingiri la Elephant Neighbours Center Jim Justus ambaye pia ni Mwanasayansi anafanya kampeni ya kuihamasisha jamii kuhusu umuhimu wa kulinda wanyapori hususan ndovu.

Justus amesema kuwa ipo haja ya jamii kuhamasishwa zaidi kuhusu faida na umuhimu wa wanyamapori ikizingatiwa kwamba kuna idadi kubwa ya ndovu imepungua mno kutokana na uwindaji haramu unaotekelezwa na wananchi hususan wanaoishi pambizoni mwa mbuga hizo.

Aidha ameendelea kusema kuwa kila aliyepata hasara kutokana na wanyamapori kuna utaratibu unaofaa kufuatwa ili muathiriwa kupata fidia.

Ni kauli iliyoungwa mkono na kamishna wa Kwale Gedion Oyagi ambaye amewasihi wakaazi kuwa mstari wa mbele kulinda raslimali yao.

Wawili hao wameyasema haya kaunti ya Kwale wakati wa matembezi hayo yanatarajiwa kukamilika tarehe 19 eneo bunge la Lungalunga.

BY EDITORIAL TEAM