HabariNews

Vijana watolewa wito kujituma kama njia ya kuepuka uhalifu.

Kuna umuhimu wa kuwahamasisha vijana kuhusu haki zao na majukumu yao katika jamii kama njia mojwapo ya kuboresha jamii.

Haya yanajiri huku baadhi ya viongozi wa dini katika kaunti ya Kwale wakisema kuwa baadhi ya vijana wanakosa kielelezo chema hivyo basi wengine hujipata katika njia isiyofaa.

Kulingana na Sheikh Amani Hamisi kutoka baraza la kidini la Inter Religious Council of Kenya kaunti ya Kwale ni sharti vijana waweze kujengwa katika sekta ya kijamii, kiuchumi na hata kidini kama njia mojawapo ya kuhakikisha wanajitenga na uhalifu.

Kwa upande wake Immaculate Mungai amewataka wazazi haswa kina mama kuzungumza na vijana wao ili waweze kuelewa changamoto zao.

Brilliant Amani ni kijana katika kaunti ya Kwale na ametoa wito kwa vijana wenzake kujituma kama njia ya kuepuka uhalifu.

BY EDITORIAL DESK