Viongozi wa kidini kaunti ya Kwale sasa wanaitaka serikali ya kitaifa kufutilia mbali mpango wa masomo ya ziada katika shule za umma na za kibinafsi.
Viongozi hao kupitia Sheikh Kassim Zani wanasema kuwa wazazi wengi hawana uwezo wa kugharamia masomo hayo kutokana na hali ngumu za kiuchumi.
Sheikh Zani amedai kwamba baadhi ya shule kaunti hiyo zimekuwa zikiwalazimisha wazazi wasiojiweza kulipa fedha za masomo ya ziada kwa wanao.
Wakati uo huo, kiongozi huyo wa kidini ametilia shaka usalama wa wanafunzi wanaotoka shuleni nyakati za usiku kwa sababu ya masomo ya ziada.
Sheikh Zani sasa anaitaka serikali kuu kuharamisha masomo hayo akisema kuwa yanatishia pakubwa usalama wa watoto wao.
BY EDITORIAL DESK