Siku kadhaa baada ya polisi kuyavamia makazi ya mwanawe rais mstaafu Uhuru Kenyatta, Jomo Muigai, rais huyo mstaafu amedai ilikuwa ni njama ya kuweka bunduki na dawa za kulevya nyumbani kwake.
Akiongea kwenye Mkutano na wahariri jijini Nairobi, Kenyatta amezungumzia bunduki zinazomilikiwa na Jomo na Muhoho akisema kuwa wanawe wawili wanamiliki bunduki 6 tatu kila mmoja.
Aidha ameweka wazi kwamba bintinye Ngina Kenyatta hana leseni ya kumiliki silaha yoyote hivyo basi hana bunduki.
Kenyatta ameongeza kuwa hakuna yeyote katika familia yake amepokea agizo la serikali kuzirudisha silaha hizo.
Ameongeza kuwa faida za kiusalama ambazo Mama Ngina ambaye ni mamaye rais huyo mstaafu ni za kutokana na cheo alichokuwa nacho mama yake cha kuwa Mama Taifa na si kwa sababu ya mamlaka aliyo nayo kutokana na cheo chake.
Amedai kuwa hata hivyo itawabidi waajiri walinzi wa usalama wa kibinafsi.