HabariNews

Familia Yaomboleza vifo vya Watoto 3 waliofariki baada ya kula uyoga wa sumu huko Bamba

Huzuni imegubika familia moja huko Bamba eneobunge la Ganze kaunti ya Kilifi baada ya watoto 3 kuaga dunia.

Watoto hao wamekumbana na mauti baada ya kula uyoga wenye sumu walioupata shambani walikokuwa wameenda kulima.

Kulingana na mzazi wa watoto hao, wanawe hao, walijitayarishia uyoga huo kisha kuula.

Inaarifiwa kuwa watoto hao baadaye walianza kulalamikia maumivu ya tumbo ambapo walipelekwa katika hospitali ya Bamba kabla ya kuhamishwa kwenye hospitali ya Kilifi.

Miili ya watoto walioga dunia inahifadhiwa katika hospitali ya rufaa ya kaunti hiyo ikisubiri kufanyiwa upasuaji.

Wakati huo huo watoto wengine wawili ambao walikula uyoga huo wa sumu wamelazwa katika hospitali ya rufaa ya Kilifi wakiendelea kupokea matibabu.

BY EDITORIAL DESK