HabariNews

Mfanyakazi anayedaiwa kumuua bosi Kilifi kufikishwa mahakamani Malindi

Mfanyakazi wa nyumbani anayedaiwa kumuua kwa kumdunga kisu Afisa mkuu wa
idara ya uchumi na raslimali za Bahari kaunti ya Kilifi Rahab Karisa
anatarajiwa kuwasilishwa mahakamani Malindi jumatano hii.

Mshukuliwa huyo ambaye amekuwa akitumia majina Tofauti la Sara na Diana
alikamatwa siku ya jumanne tarehe 25 mwezi julai eneo la Busia katika
mpaka wa Kenya na Uganda alipokuwa katika harakati za kutorokea taifa
jirani.

Inaarifiwa kuwa mshukiwa alikuwa akitoroka kwa kutumia pikipiki
aliyokuwa amekodisha kumpeleka nchini Uganda
Aidha inaarifiwa mwendesha pikipiki alipongundua kuwa alikuwa amebeba
mtu anayeshukiwa kutekeleza uhalifu na alikuwa katika harakati za
kutoroka aliwafahamisha polisi wa mpakani.

Itakumbukwa Rahab Karisa aliuawa kwa kudungwa kisu nyumbani kwake eneo
la Mnarani kaunti ya Kilifi na mfanyakazi wake huyo siku ya alhamisi
wiki iliyopita.

BY EDITORIAL DESK