Mwenyekiti wa kitaifa wa wamiliki wa matatu Albert Karakacha ameitaka serikali ya kenya Kwanza kufanya juhudi zitakazowezesha kushuka kwa bei ya mafuta ya petroli.
Kulingana na Karakacha kupanda kwa bei ya mafuta kumeathiri shughuli nyingi zilizopelekea Uchungu wa gharama ya maisha na kumwumiza mwananchi wa kawaida licha ya serikali kuahidi kupunguza gharama hio.
Akizungumza katika Kauti ya Mombasa Karakacha alidokeza kuwa kuna haja ya kuwepo kwa ushirikiano baina ya wahudumu wa matatu, abiria na mamlaka ya uchuzi na usalama Barabarani NTSA ili kudumisha usalama barabani.
”Naomba rais aone vile tutasaidia mambo ya mafuta iwe kuenda chini kwa sababu abiria wanaumia na madereva, vile walipta uongozini walisema mambo ya husla na tutazidi kukaa na serikali kusaidia mwananchi wa kawaida.”Alisema Karakacha.
Karakacha alisema mikakati kabambe imewekwa ili kudhibiti ajali za Barabarani ikiwemo kutoa mafunzo kwa madereva hasa wakati huu ambapo familia na jamaa wanaelekea katika msimu wa likizo.
Karakacha vile vile alirai mashirika ya kibiashara kutolazimisha madereva kufanya kazi kupitiliza kama njia ya kupunguza ajali Barabarani huku akiongeza kuwa watahakikisha jambo hilo linatimia.
”Madereva wakuwe waangalifu barabarani kama chama tunakuja nan ji a ya kutoa mafunzo kwa madereva ili kupunguza ajali barabarani kila sacco iweke ratiba na tunaomba dereva asikubali kuenda mara mbili akiskia amechoka anapumzika.”