Shirika la Msalaba Mwekundi limetoa onyo kuhusiana na viwango hatari vya maji katika Mto Tana.
Katika taarifa iliyotolewa hii leo ni kwamba Shrika hilo lilitoa tahadhari kwa kaunti za Kilifi, Tana River na Garissa, ilibainika kuwa kaunti hizo zinakabiliwa na hatari kubwa ya mafuriko kutokana na mto huo.
Kulingana na Taarifa hiyo viwango vya maji ya Mto Tana vinaweka maisha ya wakazi hatarini na japo Shirika hilo limeanza kuchukua tahadhari ya mapema kwa kuweka mikakati kabambe ikiwemo kutoa tahadhari za mapema kuhakikisha usalama kwa wakazi wanaoishi karibu na kingo za mto huo.
Katibu Mkuu wa Shirika la Msalaba Mwekundu Dkr. Ahmed Idris Akizungumza jjini Nairobi katika hafla ya kutathmini utayari wa taifa katika kukabiliana na mvua za elnino, alibaini kuwepo haja ya kuwekwa mikakati maalum kukabiliana na mafuriko.
Idris alisema kuwa tayari kumeshuhudiwa maafa, maejeruhi na kuharibiwa kwa mali na makazi, kuna uwezekano mkubwa idadi ya waathiriwa ikaongezeka kadri mvua inavyozidi kuongezeka.
..
Nalo Baraza la Magavana sasa linataka kaunti zipewe mabilioni ya fedha zilizokuwa zimetengewa kukabiliana na elnino ili zitumike kuwapa msaada waliokosa makazi kutokana na mafuriko.
Likiongozwa na Mwenyekiti wake, Anne Waiguru magavana wameitaka serikali ihakikishe kuwa fedha hizo zilizotengwa hapo awali zinatumika ipasavyo kuwapa hifadhi walioathirika na mvua hizo.
..
Na huku maeneo mengi ya taifa yakiendelea kushuhudia mvua kubwa, Idara ya Anga mnamo siku ya Jumatatu ilitangaza kuwa nyumba 15,264 ziliathirwa na kupanda kwa viwango vya maji vilivyopelekea watu 15 kujeruhiwa na kuangamia kwa mifugo 1,067.
Haya yanajiri huku Umoja wa Mataifa nao ukisema kuwa mvua za Elnino zitashuhudiwa hadi mwezi Aprili mwaka ujao, na kwamba athari zake huenda zikashuhudiwa kuanzia mapema 2024.