HabariNewsSiasa

Azimio kurejelea maandamano mwezi huu, Waonya polisi dhidi ya kuvuruga mipango

 

Viongozi wa mrengo wa Azimio la Umoja wametoa onyo kwa maafisa wa Polisi dhidi ya kuvuruga maandamano yao ambayo yameratibiwa kuanza rasmi tarehe 20, Mwezi huu wa Januari katika Kaunti ya Nairobi.

Wakiwa katika eneo bunge la Likoni Kaunti ya Mombasa viongozi hao wakiongozwa na Kinara wao Raila Odinga, Kinara wa Narc Kenya Martha Karua na Kalonzo Musyoka wa Wiper miongoni mwa wengine wameonya kuhusu kuvurugwa kwa maandamano yao wakisema yatakuwa na amani.

“Jamaa anaitwa Kindiki ati anatisha mimi, ati ooh Raila ajihadhari sana ati hatua itachukuliwa, tunasema katiba ya Kenya, sasa Waziri hana mamlaka ya kuamrisha polisi, lakini bwana Kindiki hujajua mimi ni nani.” Alisema Odinga.

Naye Martha Karua kinara wa Narc Kenya alikariri kutomtambua rais William Ruto huku akimtaka rais kutohangaisha waandamanaji hao kupitia amri yake kwa maafisa polisi akimuonya kuwa atawajibikia dhamana na hasara itakayotokea.

“ujumbe wangu wa kwa rais bandia, ukioa wananchi wako kwa maandamano wapatie heshima. Sheria inamekubali maandamano ukiambia polisi wasumbue wananchi wawaumize wewe ndio utalipa,” alisema.

Kinara huyo wa Narc Kenya aidha aliibua madai kuhusu kuwepo kwa njama ya kuwakamata na kuwafungulia mashtaka baadhi ya viongozi wa Azimio.

“wanajaribu kutuma polisi washike wakubwa wa Azimio. Hawawezi shika Raila hawawezi kuja kwa Martha Karua, hawaezi kwenda kwa Kalonzo wanajaribu Ledama Ole Kina. Tunawaambiwa wajaribu kumshika Kenya nzima itaenda kotini,” alisema Karua.

Wakati uo huo wametoa wito kwa Wakenya kushiriki maandamano hayo ili kuishinikiza Serikali kushughulikia hali ngumu ya kiuchumi.

“Baba ashapiga firimbi sote tuende Nairobi tukaulize serikali bandia je, pesa yetu iko wapi, pesa yetu imeenda wapi, twende tukaulize haki yetu,” alisema Karua.

BY NEWSDESK