Chama cha mawakili mjini Mombasa kwa ushirikianao na mashirika ya kijamii yasiyo ya kiserekali ukanda wa pwani yamekongamana katika mahakama ya Mombasa kupinga mazungumzo yanayopangwa kufanyika baina ya serikali na jaji mkuu nchini Martha Koome.
Wakiongozwa na rais wa chama cha wanasheria nchini Erick Theuri, mawakili hao walikemea mazungumzo hayo na kuyataja kama mbinu ya kuleta uongozi wa kibepari.
Theuri alimtaka rais Ruto kuomba msamaha kufuatia kauli zake za shutuma huku akiishinikiza serikali ikome kuingilia kati maamuzi ya idara hiyo.
“ Kama chama cha wanasheria tunachukua msimamo thabiti kuwa mazungumzo hayo hayastahili na hayana nafasi katika katiba yetu, tunashikilia kuwa Jaji mkuu asijihusishe na asishiriki katika haya mazungumzo” Alisema
Viongozi kutoka mashirika ya kijamaii ya Amnesty International na CCSNH walishilkilkia hatua ya rais kushutumu mahakama kuwa ni kinyume cha sheria na katiba ya taifa la Kenya, wakisema hakuna kiongozi yoyote aliye juu ya sheria.
“ Sote tuko na jukumu la kufuata sheria za mahakama, Rais wa taifa la Kenya amekuaakitoa matamshi ya kuingilia mahakama kwa ujumla
“ Mahakama kama Kitengo cha serikali haiwezi kuingiliwa na kitengo kingine cha serikali, kwahio tunasimama kwa sauti moja kusema kuwa wacha vigezo vinavyozuia shughuli za mahakama zikomeshwe kwa njia yeyote ile”
Kwa upande wake Seneta wa kaunti ya Mombasa Mohammed Faki ambaye pia aliwahi kuhudumu kama wakili nchini kenya alihudhuria maandamano hayo ya amani na kukosoa mamzungumzo hayo akisema yanalenga kuhujumu idara ya mahakama.
“ Ninamwabia jaji mkuu Koome kwamba hana nafasi ya mdahalo na Ruto, kama wanamalalmiko yoyote dhidi ya jaji yoyote Yule wanahaki ya kupeleka kwa judicial service commission na itachunguzwa.
Hakuna masuala ya kujifungia katika room wakisemas wanafanya mdahalo, sisi kama wananchi tutakua na imani gani ikiwa jaji wameambiwa wafanye kesi kulingana na vile Ruto anataka”
Haya yanajiri siku mooja baada ya rais William Ruto na Jaji mkuu nchini Martha Koome kuafikiana kuhusu mazungumzo baina yao jamabo amabalo limeibua hiuisia kali miongoini mwa viongozi wa kisisasa na wakererektwa wa masuala ya sheria humu nchini.