Mwanaharakati wa masuala ya kijamii na kutetea maslahi ya watu wanaoishi na ulemavu eneo la pwani Hamisa Zaja ameteuliwa na taasisi ya amani ya marekani-us. Institute of peace kutuzwa kwa juhudi zake za kushinikiza amani hapa nchini upande wa wanawake mwaka 2023.
Kulingana Na taasisi hiyo, Zaja ni miongoni mwa orodha ya mwisho ya wanawake walio mstari wa mbele kushinikiza amani barani afrika na ulimwengu kwa jumla licha ya mazingira magumu ya kuendeleza harakati zao hasa katika jamii na maeneo wanayotoka.
Zaja ambaye ni mwanzilishi Wa shirika la Coast association for people living with disability anaendeleza juhudi za kuwasaidia vijana kwa kuwapa njia mbadala ili wasitumike na makundi ya kihalifu katika kaunti ya Mombasa ambayo inashuhudia utovu wa usalama ambapo vijana wenye umri mdogo wa hadi umri wa miaka 13 wakitumika.
Vile vile wanawake wengine Katika orodha hiyo Ni pamoja Na Daktari Marie Marcelle kutoka nchini Haiti, Abir Haj Ibrahim Wa Syria Na Petronille Vaweka kutoka Demokrasia ya Congo, DRC.
Hafla ya wanawake hao kutuzwa inatarajiwa kufanyika mwezi ujao Wa Februari Katika Jiji la Washington DC nchini Marekani.
BY MAHMOOD MWANDUKA