HabariMazingiraMombasa

UKARABATI WA MABOMBA YA MAJI TAKA KAUNTI YA MOMBASA WAENDELEA ….

Huenda kilio cha kutaka kukarabatiwa kwa mabomba ya maji taka katika kisiwa cha Mombasa kikazikwa katika kaburi la sahau baada ya kaunti yaMombasa kuanza kukarabati mambomba hayo.

Akiongea na sauti ya Pwani fm katika mahojiano ya kipekee, mkurugenzi wa kampuni maji ya mitaro Mombasa MOWASCO, Athony Njaramba, amesema kuwa tayari kaunti imeanza kujenga mabomba mapya ya maji taka sawia na kurekebisha yale ya zamani ambayo yameharibika ili kutatua tatizo hilosugu.

Aidha Njaramba amesema kufuatia agizo la gavana Joho,tayari wameweka kikosi maalum kitakachowakamata watu wanaunganisha mabomba kinyume cha sheria na kusababisha kuziba kwa maji taka.

BY NATASHA TALU